Twitxy Saved

#ChangeTanzania

Verified account This account is verified. Learn more

@ChangeTanzania

This is #ChangeTanzania movement of citizens exercising their right to #FreedomOfExpression | for activism contact via WhatssApp & Telegram +1 (862) 438-3337
Tanzania forms.gle/1JbJ9n38cpsSu5… Joined January 2012
1.3K Following 317K Followers 110K Posts

Latest posts 5

Pinned post

#ChangeTanzania Verified account @ChangeTanzania
Report ya Chande imepikwa na watu wasiojua hesabu

Wamesema kuna vifo 518 nchi nzima
Wakasema vimetoka mikoa ya

Dar. 182
Mwanza 90
Mbeya. 80
Arusha. 53

Jumla 405

Hii ni tofauti na 518 kwa 113 , hili gap ni kubwa sana ina maana namba ilitugwa tu

Kisha wakasema kuhusu maiti ni 518

Maiti zilizotambulika. 485
Ambazo hazikutambulika. 9
Jumla. 494

Kuna tofauti ya 518 - 494 = 24

Ina maana maiti 24 zimepotea ni gap kwenye report

Hii ni report wamekaa nayo kwa siku 153 inatoka ikiwa na makosa makubwa hivi

Hii ni ishara wametengeneza report tena bila umakini wowote
66 replies 152 reposts 456 likes 49K views View on X
#ChangeTanzania Verified account @ChangeTanzania
WHY THE PROPOSED RECONCILIATION PROCESS IN TANZANIA LACKS CREDIBILITY

The current reconciliation framework proposed by the Tanzanian government is fundamentally flawed, lacks practical viability, and serves as a barrier to genuine justice and accountability.
More than a year after the deadly state crackdown following the contested October 29, 2025 general election—which left over 500 citizens dead according to official figures and hundreds more facing politically motivated treason charges—the administration’s push for a state-led reconciliation commission attempts to bypass accountability rather than deliver it.

A CRITICAL ASSESSMENT
Reconciliation Without Accountability Is Unviable. Genuine transitional justice requires an independent break from the structures responsible for state violence. Historical benchmarks show that credible reconciliation succeeds only after a fundamental political transition, not while the implicated administration retains unchecked control.

Persistent Impunity for October 29, 2025. Over a year later, not a single security official has been prosecuted for the unlawful killings, enforced disappearances, or torture documented by Human Rights Watch and Amnesty International. You cannot credibly preach national healing while key opposition leaders like Tundu Lissu remain criminalized and families are barred from holding public memorials.

Elite Co-optation Over Substantive Reform. Closed-door consultations with select political figures—often reduced to meeting allowances and rubber-stamped endorsements—lack substantive debate and cannot replace structural constitutional reform.
Exclusion of Victims and the Public. Any process designed from the top down without the direct participation of victims' families, civil society, and ordinary citizens lacks public legitimacy.
A Compromised Electoral Environment. Meaningful constitutional referendums or democratic transitions are impossible under an electoral framework that disqualified major opposition candidates in 2025 and continues to restrict political freedoms.
Reversing the Burden of Justice. True reconciliation demands state acknowledgment, truth-telling, reparations, and institutional reform. Forcing aggrieved citizens to solicit apologies from perpetrators while state repression continues violates every global standard of justice.

HOW GENUINE RECONCILIATION WORKS: 10 HISTORICAL EXAMPLES
According to the International Center for Transitional Justice (ICTJ), trusted reconciliation protocols rely on four pillars: Truth-Seeking, Criminal Accountability, Reparations, and Institutional Reform

Across history, these 10 countries achieved broad citizen trust and international credibility:

1. South Africa (1996–1998)
Mechanism: Truth and Reconciliation Commission (TRC)
Why It Gained Trust: Followed the end of Apartheid; featured televised public hearings, conditional amnesty only in exchange for full public truth, and deep moral credibility led by Archbishop Desmond Tutu.

2. Rwanda (1994–2012)
Mechanism: Gacaca Courts & ICTR
Why It Gained Trust: Combined international prosecutions of top genocide architects with community-level restorative courts that prioritized truth-telling and rebuilding social cohesion after regime change.

3. Argentina (1983–1984)
Mechanism: CONADEP (National Commission on the Disappearance of Persons)
Why It Gained Trust: Established immediately after the fall of the military junta; its landmark Nunca Más ("Never Again") report led directly to the historic trial and conviction of top military commanders.

4. Chile (1990–2004)
Mechanism: Rettig & Valech Commissions
Why It Gained Trust: Conducted after Augusto Pinochet stepped down; documented thousands of killings and torture cases, leading to lifelong state pensions for survivors and eventual prosecutions of military officers.

5. Sierra Leone (2002–2004)
Mechanism: Truth and Reconciliation Commission & Special Court
Why It Gained Trust: Operated alongside a UN-backed war crimes court, ensuring that while community reconciliation took place, top warlords faced strict international justice.

6. Timor-Leste (2002–2005)
Mechanism: CAVR (Commission for Reception, Truth and Reconciliation)
Why It Gained Trust: Formed after independence from Indonesian occupation; combined grassroots community reconciliation agreements with a rigorous, internationally praised truth report.

7. Peru (2001–2003)
Mechanism: Truth and Reconciliation Commission (CVR)
Why It Gained Trust: Established after the collapse of Alberto Fujimori’s authoritarian regime; held public hearings across rural regions and laid the groundwork for Fujimori’s conviction for human rights abuses.

8. Germany (1945–1990s)
Mechanism: Nuremberg Trials & Post-1989 Stasi Archives
Why It Gained Trust: Built global standards for accountability through criminal trials, massive financial reparations, mandatory historical education, and opening secret police files to citizens after the fall of the Berlin Wall.

9. Colombia (2016–Present)
Mechanism: Special Jurisdiction for Peace (JEP) & Truth Commission
Why It Gained Trust: Created through an internationally verified peace accord; requires perpetrators from both state forces and rebel groups to confess crimes directly to victims to avoid prison sentences.

10. The Gambia (2018–2021)
Mechanism: Truth, Reconciliation and Reparations Commission (TRRC)
Why It Gained Trust: Launched after the ouster of longtime dictator Yahya Jammeh; broadcast live hearings that exposed state death squads and led to concrete government commitments to prosecute perpetrators.

CONCLUSION
In every single case, credible reconciliation happened after an authoritarian regime fell, a peace treaty stripped perpetrators of unchecked power, or an independent international body guaranteed protection for victims. Until the Tanzanian administration ends political prosecutions, holds perpetrators of the October 29 violence accountable, and guarantees independent constitutional reform, this strategy represents a grave lapse in judgment and warrants unified public opposition.
#ChangeTanzania Verified account @ChangeTanzania
KWA NINI MCHAKATO WA MARIDHIANO UNAOPENDEKEZWA TANZANIA HAUNA UHALALI

Pendekezo la sasa la maridhiano linaloongozwa na serikali ya Tanzania lina kasoro za kimsingi, halitekelezeki kivitendo, na linatumika kama kizuizi cha haki ya kweli na uwajibikaji.

Zaidi ya mwaka mmoja baada ya ukandamizaji wa kikatili uliofuatia uchaguzi mkuu wenye utata wa Oktoba 29, 2025—ambao ulisababisha vifo vya zaidi ya raia 500 kwa mujibu wa takwimu rasmi na mamia wengine kufunguliwa mashtaka ya kisiasa ya uhaini—hatua ya utawala wa sasa kuunda tume ya maridhiano inalenga kukwepa uwajibikaji badala ya kuuleta.

TATHMINI YA KINA
Maridhiano Bila Uwajibikaji Hayawezekani. Haki ya mpito ya kweli inahitaji kujitenga kisheria na kimuundo na mifumo iliyohusika na ukatili wa dola. Historia inaonyesha kuwa maridhiano yenye kuaminika hufanikiwa baada ya mabadiliko ya kisiasa au kikatiba, si wakati utawala unaotuhumiwa ukiwa bado na mamlaka yasiyodhibitiwa.

Kukosekana kwa Uwajibikaji kwa Matukio ya Oktoba 29, 2025. Zaidi ya mwaka mmoja umepita bila ofisa yeyote wa vyombo vya usalama kufikishwa mahakamani kwa mauaji, utekaji nyara, na mateso yaliyoripotiwa na Human Rights Watch na Amnesty International. Huwezi kuhubiri uponyaji wa kitaifa huku viongozi wakuu wa upinzani kama Tundu Lissu wakiendelea kuandamwa na kesi za kisiasa na familia zikizuiwa kufanya kumbukumbu za wapendwa wao.

Mazungumzo ya Wateule Wachache Badala ya Mageuzi ya Kweli. Mikutano ya faragha na wanasiasa wachache—ambayo mara nyingi hugubikwa na posho za vikao na maazimio yaliyoandaliwa tayari—haina mijadala huru na haiwezi kuchukua nafasi ya Katiba Mpya.

Kuwaweka Kando Wahanga na Wananchi. Mchakato wowote unaopangwa kutoka juu bila ushiriki wa moja kwa moja wa familia za wahanga, asasi za kiraia, na wananchi wa kawaida unakosa uhalali wa umma.
Mazingira Mabovu ya Uchaguzi. Kura ya maoni ya haki au mabadiliko ya kidemokrasia hayawezekani chini ya mfumo wa uchaguzi uliowaengua wagombea wakuu wa upinzani mwaka 2025 na unaoendelea kuminya uhuru wa kisiasa.

Kupindua Misingi ya Haki. Maridhiano ya kweli yanahitaji serikali kukiri makosa, kusema ukweli, kutoa fidia, na kufanya mageuzi ya kitaasisi. Kuwalazimisha wahanga waombe msamaha kutoka kwa watesi wao huku ukandamizaji ukiendelea ni kinyume na viwango vyote vya kimataifa vya haki.

JINSI MARIDHIANO YA KWELI YANAVYOFANYIKA: MIFANO 10 YA KIHISTORIA
Kwa mujibu wa Kituo cha Kimataifa cha Haki ya Mpito (ICTJ), michakato ya maridhiano inayoaminika hutegemea nguzo nne:

Kutafuta Ukweli, Uwajibikaji wa Kisheria, Fidia, na Mageuzi ya Taasisi.

Kihistoria, nchi hizi 10 zilifanikiwa kupata imani ya wananchi na jumuiya ya kimataifa:

1. Afrika Kusini (1996–1998)

Mfumo: Tume ya Ukweli na Maridhiano (TRC)

Kwa Nini Iliaminika: Iliundwa baada ya kuanguka kwa utawala wa ubaguzi wa rangi (Apartheid); ilifanya vikao vya wazi vilivyorushwa moja kwa moja kwenye runinga, ilitoa msamaha kwa sharti la kusema ukweli wote hadharani, na iliongozwa na Askofu Mkuu Desmond Tutu aliyekuwa na uadilifu mkubwa.

2. Rwanda (1994–2012)

Mfumo: Mahakama za Gacaca na Mahakama ya Kimataifa (ICTR)

Kwa Nini Iliaminika: Iliunganisha mashtaka ya kimataifa dhidi ya viongozi wakuu wa mauaji ya kimbari na mahakama za kijamii (Gacaca) zilizolenga ukweli na kujenga upya mshikamano wa jamii baada ya mabadiliko ya utawala.

3. Argentina (1983–1984)

Mfumo: Tume ya Kitaifa ya Watu Waliopotezwa (CONADEP)
Kwa Nini Iliaminika: Iliundwa mara tu baada ya kuanguka kwa utawala wa kijeshi; ripoti yake maarufu ya Nunca Más ("Kamwe Tena") ilipelekea kufunguliwa mashtaka na kufungwa kwa makamanda wakuu wa jeshi.

4. Chile (1990–2004)

Mfumo: Tume za Rettig na Valech
Kwa Nini Iliaminika: Ziliundwa baada ya dikteta Augusto Pinochet kuondoka madarakani; ziliweka wazi maelfu ya visa vya mauaji na mateso, na kupelekea manusura kulipwa pensheni ya maisha na maofisa wa jeshi kushtakiwa.

5. Sierra Leone (2002–2004)

Mfumo: Tume ya Ukweli na Maridhiano na Mahakama Maalum

Kwa Nini Iliaminika: Ilifanya kazi sambamba na mahakama ya uhalifu wa kivita iliyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, kuhakikisha kuwa wakati maridhiano ya kijamii yakifanyika, wababe wa kivita wanakabiliwa na mkono wa sheria.

6. Timor-Leste (2002–2005)

Mfumo: Tume ya Mapokezi, Ukweli na Maridhiano (CAVR)

Kwa Nini Iliaminika: Iliundwa baada ya nchi kupata uhuru; iliunganisha makubaliano ya maridhiano katika ngazi ya vijiji na ripoti madhubuti ya ukweli iliyosifiwa kimataifa.

7. Peru (2001–2003)

Mfumo: Tume ya Ukweli na Maridhiano (CVR)

Kwa Nini Iliaminika: Iliundwa baada ya kuanguka kwa utawala wa kimabavu wa Alberto Fujimori; ilisikiliza ushuhuda wa wananchi vijijini na kuweka msingi uliopelekea Fujimori kuhukumiwa kifungo kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.

8. Ujerumani (1945–Miaka ya 1990)

Mfumo: Mahakama za Nuremberg na Kufunguliwa kwa Nyaraka za Stasi

Kwa Nini Iliaminika: Iliunda viwango vya kimataifa vya uwajibikaji kupitia kesi za jinai, malipo makubwa ya fidia, elimu ya lazima ya historia, na kufungua mafaili ya polisi wa siri kwa wananchi baada ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlin.

9. Colombia (2016–Sasa)

Mfumo: Mahakama Maalum ya Amani (JEP) na Tume ya Ukweli

Kwa Nini Iliaminika: Iliundwa kupitia mkataba wa amani uliosimamiwa kimataifa; inawalazimu wahusika kutoka vyombo vya dola na waasi kukiri makosa yao moja kwa moja mbele ya wahanga ili kuepuka vifungo virefu.

10. Gambia (2018–2021)

Mfumo: Tume ya Ukweli, Maridhiano na Fidia (TRRC)

Kwa Nini Iliaminika: Ilianzishwa baada ya kuondolewa madarakani kwa dikteta Yahya Jammeh; ilirusha mubashara ushuhuda uliofichua vikosi vya mauaji vya serikali na kupelekea serikali kuahidi kuwashtaki wahusika wote.

HITIMISHO
Katika kila mfano kati ya hizi 10, maridhiano yenye kuaminika yalifanyika baada ya utawala wa kimabavu kuanguka, mkataba wa amani kupunguza nguvu za watesi, au chombo huru cha kimataifa kudhamini usalama wa wahanga. Hadi serikali ya Tanzania itakapofuta kesi za kisiasa, kuwawajibisha waliohusika na mauaji ya Oktoba 29, na kuruhusu mchakato huru wa Katiba Mpya, mkakati huu ni kosa kubwa la kiuongozi na unapaswa kupingwa na wananchi wote.
0 replies 8 reposts 12 likes 692 views View on X