Twitxy Saved

The Chanzo

Verified account This account is verified. Learn more

@TheChanzo

We Are Bilingual Multimedia Storytellers Looking At The World From Ground Up. Una habari? WhatsApp/Telegram 0753815105
Dar es Salaam, Tanzania thechanzo.com Joined August 2020
195 Following 81K Followers 14K Posts

Latest posts 5

The Chanzo Verified account @TheChanzo
Angel Wariael, binti aliyejeruhiwa Oktoba 29, afariki dunia Muhimbili

Dar es Salaam. Angel Wariael,13,  binti aliyekuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutokana na kujeruhiwa na risasi kwenye matukio ya Oktoba 29 akiwa nyumbani kwao Manzese amefariki dunia.

Hospitali imethibitisha kifo chake leo Novemba 18, 2026, kupitia Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Irene Charles Mbonde, pamoja na taarifa kutoka kwa mmoja wa wanafamilia.

Katika taarifa  kwa waandishi wa habari, Hospitali ya Taifa Muhimbili, (MNH) imetoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huo, ikiwaombea nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu.

Oktoba 31, 2026, The Chanzo, iliripoti taarifa ya Angel na mama yake mzazi kuhitaji msaada ikiwemo wa  matibabu kutokana na hali ya afya yake iliyomsababisha kukatisha masomo. Kufuatia taarifa hiyo, alipatiwa msaada na kuanza matibabu Muhimbili hadi mauti yalipomkuta.
11 replies 30 reposts 133 likes 3.2K views View on X