Saleh Khamis, mmoja wa washukiwa watatu wa ulanguzi wa dawa za kulevya waliokamatwa siku ya Jumapili katika kaunti ya Kwale, ametajwa na DCI kama mfanyabiashara mkubwa wa dawa za kulevya anayetafutwa na mamlaka za Kenya na Tanzania.
Mashahidi watatu wamejitokeza mbele ya Mahakama ya Nairobi kutoa ushahidi dhidi ya Sammy Murigi Maina, dereva wa matatu anayekabiliwa na mashtaka ya kusababisha ajali iliyogharimu maisha ya abiria watatu katika Barabara ya Enterprise.
Mahakama ya Makadara imewaagiza maafisa kadhaa wa usalama kufika mahakamani Novemba 13 kuhojiwa kuhusu madai ya vitisho dhidi ya Wakili Abshir Ahmed-sadak Abdi anayedaiwa kutekwa nyara.
Watu watatu bado hawajulikani waliko licha ya kufungwa kwa operesheni ya utafutaji na uokoaji katika jengo lililoporomoka Eastleigh, huku serikali ikisisitiza kuwa hakuna miili mingine iliyopatikana kwenye vifusi.