Katika Siku ya Askari Wastaafu (Veterans Day), tunawatambua na kuwaenzi Wamarekani waliotumikia katika Vikosi vya Ulinzi vya Marekani na kuheshimu kujitolea kwao, ujasiri wao na kujitoa kwao mhanga katika kulinda taifa letu na uhuru wetu.
Utumishi wao unaonyesha dhamira ya kudumu ya kuzingatia misingi inayotuunganisha na kulinda haki na uhuru tunaouthamini.
Ubalozi wa Marekani utafungwa Jumatano, tarehe 11 Novemba, kuadhimisha siku hii. Tunawashukuru wote waliotumikia katika vikosi vyetu vya ulinzi.